BAADHI ya wanafunzi wa shule za msingi  na sekondari  mkoani 
Lindi, wameulalamika  utaratibu wa mgao wa walimu ambao wake za vigogo 
na walimu wenye sifa, wanarundikwa katika shule za mijini.
Utaratibu huo unasababisha kukosekana kwa uwiano katika utaoji wa elimu baina ya shule za mijini na vijijini.
Wanafunzi hao walitoa malalamikoa hayo juzi 
kupitia Baraza la Watoto la Wilaya ya Kilwa, lilipokuwa 
likizungumza na timu ya waandishi wa habari waliotembelea baraza hIilo
 kwa  ufadhili wa Shirika la Save the Children.
Akizungumza kwa  niaba ya baraza la watoto la 
wilaya hiyo, Idrisa  Samli,  alisema moja ya  kero na sababu 
zinazochangia  kuzohofisha morali ya watoto kutopenda shule, ni pamoja 
na kitendo cha watendaji na viongozi  wa halmashauri  hiyo, kutoa 
upendeleo kwa ndungu na wake zao, kufundisha shule za mijini.
Samli alisema kitendo hicho  ndiyo chanzo cha 
kukithiri kwa tatizo la utoro miongoni mwa wanafunzi na tofauti katika 
uatoaji wa elimu kati ya shule za mjini na vijiji .
Alielezea kushangazwa kwake kuona viongozi wa 
elimu katika wilaya hiyo, hawalichukulii suala hilo kama sehemu ya 
matatizo yanayochangia kushusha  kiwango cha taluuma.
Baraza hilo limeuomba uongozi wa wilaya,  
kuangalia uwezekano wa kuwapunguza walimu wanaofundisha  mijini na 
kuwapeka vijiji ambako kuna  upungufu mkubwa wa walimu.
Limesema hatua hiyo itasaidia kuleta wiano wa walimu na wanafunzi katika shule za mijini na vijijini.
No comments:
Post a Comment