Friday, November 16, 2012

DRC KUULINDA MJI WA GOMA.

Wanajeshi wa CongoGavana wa jimbo la kivu kaskazini Julien Paluku amesema wapiganaji hao wa waasi wa M23 walikuwa wamempigia simu kumjulisha kuwa watawasili leo usiku mjini Goma.
Paluku amesema wanajeshi 150 wa waasi wameuawa lakini msemaji wa waasi hao amekanusha habari hizo.
Mapigano hayo ndiyo mabaya zaidi tangu mwezi Julai mwaka huu katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini.
Zaidi ya watu laki tano wamehama makwao tangu mwezi Aprili mwaka huu, wakati wanajeshi kadhaa walipoasi kutoka kwa jeshi la Serikali.
Mapigano hayo yamekuwa yakiendelea karibu na kijiji cha Kibumba takriban kilomita 30 Kaskazini mwa Goma.

No comments:

Zilizosomwa zaidi