Baada ya fununu nyingi kusambaa mtaani kuwa staa wa Bongo Fleva, Raheem Nanji ‘Bob Junior’ kuwa ni Shoga sasa ameogea waziwazi.
Akizungumza kupitia kipindi cha runinga moja usiku wa Ijumaa
iliyopita, Bob Junior alisema chanzo cha yeye kudaiwa ni shoga ni wimbo
wake maarufu wa Oyoyo.
Alisema
mara baada ya kuitoa video ya wimbo wake huo akiwa anakata sana mauno,
watu walikuwa wakimpigia simu, wengine wakimtumia meseji kwamba,
anaonekana ni ‘chakra’ maana anayaweza sana mauno.
“Watu wanasema
mimi ni shoga, lakini si kweli. Kisa kilianzia kwenye ule wimbo wangu wa
Oyoyo. Unajua katika video ya ule wimbo nilikata sana mauno, watu
wakaamini mimi shoga."
“Wengine walikuwa wakinitumia hata meseji
wakiamini hivyo. Kwa hiyo sababu kubwa ni ile video tu, watu wana mambo
ya ajabu sana,” alisema Bob Junior huku watu alioongozana nao usiku
huo wakitingisha vichwa kukubaliana naye.
Ishu ya Bob Junior
kuonekana ni chakra pia iliwahi kusababisha amfikishe kortini kwenye
Mahakama ya Mwanzo Kinondoni, Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu akidaiwa
kumtukana msanii huyo matusi ya nguoni likiwemo hilo la ushoga.
Katika
kesi hiyo iliyofikishwa kwenye mahakama hiyo kwa mara ya kwanza Mei 4,
2011 na kusikilizwa na Hakimu Mfawidhi Mariam Masamalo, Wema
alihukumiwa kulipa faini ya shilingi 40,000 au kwenda jela miezi 6
ambapo alifanikiwa kulipa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Zilizosomwa zaidi
-
-
Katibu Mkuu wa CCM Abd...
-
-
...
-
Kundi la kigaidi la Al-Shabaab limetibitisha kuwa kiongozi wao Ahmed Abdi Godane aliuawa siku ya Jumatatu katika shambu...
No comments:
Post a Comment