Serikali ya Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo, imetupilia mbali matakwa yaliyotolewa na
wapiganaji wa waasi wa kuanzisha mazungumzo ya amani, na kukariri kuwa
itaendelea kuulinda mji wa Goma, Mashariki mwa nchi hiyo.
Waasi wa M23 wamesemekana kuukaribia mji huo huku maelfu ya raia wakikimbia makwao.Mapema hii leo, wapiganaji hao walitoa ilaani ya saa ishirini na manne kwa serikali ya nchi hiyo kuanzisha mazungumzo, ya amani la sivyo wataendelea na vita hivyo.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa limelaaini hatua hiyo ya waasi wa M23 ya kuendelea na mapigano huku wakielekea mji wa Goma.
Mapigano hayo yametajwa kuwa mabaya zaidi tangu mwezi Julai Mwaka huu katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini.
Barabara za mji wa Goma hazikuwa na raia kama kawaida na magari ya kijeshi na yale ya umoja wa mataifa ndiyo yaliyokuwa yakizunguka mji huo.
No comments:
Post a Comment