WATUHUMIWA wa kuharibu na kuchoma moto
makanisa huko Mbagala jijini Dar es Salaam, mapema leo wamefikishwa
mbele ya Hakimu Binge Mashabala wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Watuhumiwa hao watano wamesomewa
mashtaka matano na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka,
yanayowahusisha na njama za kutenda makosa, kuvunja majengo, uharibifu
na wizi wa vifaa vya makanisa na kusabisha hasara ya milioni 550/=.
Washitakiwa hao, Shabani Hamisi, Issa
Abdullah, Kambi Haji, Hamadi Mahambo na Wajabali Julius, walikana makosa
hayo na kesi kuahirishwa hadi Oktoba 30 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment