Saturday, September 29, 2012

Somalia

Masheikh wa Somalia waomba ulalamikaji wa amani juu ya filamu dhidi ya Uislam

  •  
Watumishi wa Kiislamu nchini Somalia walipinga vikali filamu huru inayomkashifu Mtume Muhammad, lakini walitaka kuwepo na maandamano ya kujizuia na ya amani yanayoendana na mafunzo ya Kiislamu.
  • Wasomali mjini Mogadishu wakinyanyua juu Koran huku wakionesha mabango ya kupinga filamu iliyomwonesha Mtume Muhammad na Waislamu katika njia isiyo ya heshima. [Na Mahmoud Mohamed/Sabahi]
    Wasomali mjini Mogadishu wakinyanyua juu Koran huku wakionesha mabango ya kupinga filamu iliyomwonesha Mtume Muhammad na Waislamu katika njia isiyo ya heshima. [Na Mahmoud
Sheikh Hassan Abdirahman wa Mogadishu alisema masheikh wa Somalia wanapinga vikali filamu hiyo huru yenye jina la "Kutokuwa na hatia wa Waislamu", ambayo inamkashifu Mtume na Uislamu kwa jumla.
"Mtume, amani iwe juu yake, ana pahali maalumu katika nyoyo za Waislamu," Abdirahman aliiambia Sabahi. Alisema kuwa kumheshimu Mtume ni jambo la lazima kwa Waislamu, lakini akasisitiza umuhimu wa kuilinda dini katika njia ya busara na hekima, kuliko kutumia vurugu kama njia ya kuonesha hasira.
"Tabia yetu katika hili lazima iwe ya busara na mapatano yanayoendana na mafundisho na misingi ya Kiislamu, unaopinga vurugu na uharibifu," alisema. "Tunaonya dhidi ya matumizi ya vurugu na ushari dhidi ya watu wasio na hatia kama njia ya kuonesha hasira, kwa sababu kuua nafsi zisizo na hatia na kuharibu mali au kuwashambulia wengine hakuendani na mafundisho ya Kiislamu."
"Utumiaji mguvu, uharibifu wa kishenzi na uharibifu wa mali, pamoja na kuua watu wasio na hatia kwa kushambulia makao makuu ya balozi na kuwalenga watalii -- mambo yaliyotokea katika baadhi ya nchi za Kiarabu --- hakuwezi kuwa suluhisho kwa tatizo hili," Abdirahman alisema.
Kama jawabu ya kutolewa kwa filamu hiyo mitandaoni wiki iliyopita, waandamanaji walivamia balozi za Marekani huko Misri, Libya na Yemen, na maandamano ya vurugu yalizuka sehemu nyengine katika ukanda huo. Balozi wa Marekani nchini Libya Christopher Stevens na wafanyakazi wa kidiplomasia wengine watatu waliuliwa katika mashambulizi kwenye Ubalozi wa Marekani huko Benghazi.
Makamu mwenye kiti wa Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu nchini Somalia Sheikh Nur Barud alisema kuwakashifu Waislamu kusichukuliwe kama ni uhuru wa maoni. "Uhuru wa maoni haumaanishi kukiuka utakatifu wa kidini," aliiambia Sabahi.
Alisema kuwa filamu hiyo ni tendo la uchokozi uliokusudiwa kuwakashifu Waislamu na kushambulia maadili yao, pamoja na kuchochea chuki baina ya Waislamu na Wakristo.
"Sisi katika Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu nchini Somalia tunapinga vikali filamu hii ambayo inamkashifu Mtume Muhammad na dini ya Kiislamu. Tunapenda pia kuelezea kukerwa kwetu na kutukanwa mfululizo kwa kile tunachoamini kuwa ni kitakatifu kwetu," alisema.
Barud alisema nchi za Kiislamu zinapaswa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya filamu hii kuliko kutumia nguvu dhidi ya watu wasio na hatia. "Waislamu lazima wawashtaki watu binafsi na asasi ambazo zilihusika na utolewaji wa filamu hii inayokera katika mahakama za kimataifa kuliko kufanya tendo lolote ambalo lina madhara kwa Waislamu na kuharibu kesi yao," alisema.
"Tusiwahusishe watu wasio na hatia kwa matendo yaliyofanywa na mwenye makosa kwa sababu kuua na kuwashambulia watu wasio na hatia ni kitu ambacho Uislamu unakipinga," alisema.
Sheikh Mohamed Aden Kheyrow, mkurugenzi mkuu wa Wizara ya Masuala ya Kiislamu na Mali ya Wakfu ya Somalia, alisema serikali ya Somalia inakataa aina yoyote ya kuukashifu Uislamu.
"Kushambulia maadili yetu ya Kiislamu na kumtukana Mtume wetu hakukubaliki," aliiambia Sabahi. "Kwa maneno makali kabisa yanayowezekana, tunalaani filamu hii ambayo inamkashifu Mtume Muhammad."
Kheyrow alisema waandamanaji wanapaswa kufungamana na haki ya kuandamana kwa amani na kujizuia kushambulia balozi. "Uislamu unapinga vurugu na uharibifu, na ndio maana waandamanaji wa Kiislamu wanapaswa waandamane kwa amani na hisia zao lazima ziwe za hekima na busara," alisema. "Wasiwashambulie wageni na balozi katika nchi zao."





















































































No comments:

Zilizosomwa zaidi