Monday, August 27, 2012

Kituko kimetokea mkoani Tabora baada ya ziara ya kushtukiza iliyofanywa na mkuu wa mkoa katika stendi ya mabasi ya mkoa huo. Katika usiku wa kuamkia siku ya Sensa mkuu wa mkoa huo Bi Fatuma Mwasa aliitembelea stendi hiyo na kuikuta ina uchafu usioelezeka jambo lililomfanya bi Fatuma kuwakurupusha Watendaji wa wilaya ya Tabora mjini usiku huo kufika na kuanza kufanya usafi mara moja, muda huohuo. Kwa aibu waliyoipata watendaji hao, waliamua kuwapa tenda vijana wakafanya usafi ndani ya stendi usiku huo.

No comments: