Saturday, April 2, 2016

UJUE UTARATIBU WA KUDAI FIDIA YA BIMA KWA ABIRIA ALIYEPATA AJALI


UTARATIBU WA KUDAI FIDIA YA BIMA KWA ABIRIA ALIYEPATA AJALI (CLAIM PROCEDURE)
Abiria anapaswa kuandika barua kwenda kampuni husika ya bima iliyokatiwa hilo Bus. Katika barua hiyo aambatanishe vifuatavyo;

1. TIKETI YA SAFARI.
2. CHETI CHA MATIBABU YA HOSPITALI.
3. FOMU YA POLISI (PF 3).
4. MCHANGANUO WA GHARAMA ALIZOINGIA.
5. PF 90.
6. PF115

7. TIKETI YAKE kama bado anayo (kama imepotea kutokana na mazingira ya ajali itaeleweka haina shida sana). Cha muhimu ni kwamba kama hakuzidiwa sana basi ahakikishe yeye mwenywe kuwa jina lake lipo kwenye orodha ya majina ya polisi ya majeruhi kwa kutaja majina yake yote kamili.

8. Cheti cha kifo, ikiwa unadai kwa niaba ya ndugu aliyefariki katika ajali.

9. Hakikisha unaziwasilisha nyaraka hizi kwenye ofisi ya bima husika.
KUMBUKA: Utalipwa tu iwapo,ulipanda magari ambayo yaliruhusiwa kubeba abiria tu (PSV) yaani Passenger Service Vehicles kama vile mabasi ya abiria,daladala, na taxi zilizosajiliwa.

NB: Kampuni ya bima ikikataa kulipa madai unayoona ni halali, wasilisha mgogoro wako katika ofisi za Msuruhishi wa Migogoro ya Bima zilizopo PPF Tower Dar es salaam au ofisi ya Mamlaka ya Bima(TIRA) zilizopo nchi nzima.

No comments:

Zilizosomwa zaidi