Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi,
Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi wa Bwana Assad ulianza Novemba
5, mwaka huu, 2014.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Bwana Assad ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 2, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.
Kabla ya
uteuzi wake, Bwana Assad alikuwa Profesa Mshiriki, Idara ya Uhasibu,
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Bwana Ludovick Utouh
ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma.
Profesa
Assad ni msomi, mwenye weledi, ujuzi na uzoefu mkubwa wa uhasibu na
udhibiti wa fedha ambaye ana Shahada ya Uzamivu wa Uhasibu (PHD in
Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Southampton, Uingereza mwaka 2001 na
Shahada ya Uzamivu katika Udhibiti wa Fedha (MA in Financial Accounting)
kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City, Jamhuri ya Ireland mwaka 1991.
Profesa
Assad pia ana Stashahada ya Kitaaluma ya Uhasibu (Professional Diploma
in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City mwaka 1990 na Shahada
ya Biashara (Bachelor of Commerce) ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam mwaka
1988.
Pamoja na
uzoefu wa kitaaluma, Profesa Assad anao uzoefu mkubwa katika eneo la
uhasibu na ukaguzi. Alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi
(NBAA) kwa miaka saba (2007 - 2014); ni Rais na Mjumbe wa Chama cha
Wahasibu Afrika (Pan African Federation of Accountants) tangu mwaka
2012; na ni mjumbe wa Bodi kadhaa za Wakurugenzi nchini Tanzania.
Katika
kumteua Profesa Mussa Juma ASSAD kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali, Rais anayo imani kubwa kuwa elimu, weledi, ujuzi na uzoefu
ambao Profesa Assad anao utamwezesha kutekeleza vema majukumu ya nafasi
hiyo muhimu sana katika utawala bora wa nchi yetu.
No comments:
Post a Comment