WALIMU
wa shule ya sekondari ya Kihesa iliyopo manispaa ya iringa wameendesha
mgomo wa siku mbili kutoingia madarasani kufundisha wakimshinikiza Ofisa
elimu taaluma manispaa ya iringa kufika shuleni hapo na kumuondoa
mwanafunzi aliyefukuzwa shule na bodi kwa makosa ya utomvu wa nidhamu.
Mgomo huo ulichukua takribani masaa sita shuleni hapo ambapo Mwanafunzi huyo aliyetambulika kwa jina Lomina Chengula kidato cha Pili D akiwa na wenzake mapema mwezi huu alisimamishwa masomo na uongozi wa bodi ya shule hiyo kwa makosa yasiyovumilika, lakini kioja kilijitokeza pale ofisa elimu taaluma huyo kuchukua jukumu la kumrejesha shuleni mwanafunzi huyo kwa nguvu.

Awali
katika sakata la utovu wa nidhamu walikuwa wanafunzi tisa na bodi
iliamua kuwarejesha wanafunzi tisa kwa masharti maalumu na kati ya hao
tisa wengine wapo madarasani hadi sasa na stafu ya kihesa haina tatizo
na hao wanafunzi kutokana na bodi kuamuru warudi shuleni,ila lililoleta
msuguano hapo ambalo linapelekea walimu kutoingia madarasani mpaka
watakapopata ufumbuzi wa swala hilo ni juu ya binti mmoja ambae bodi ya
shule ambae ndiyo mwakilishi wa kamishina wa elimu iliamuru uyo binti na
wenzake kwa sababu walikuwa katika makundi wasimamishwe shule ofisa
elimu taaluma kwa mamlaka yake na sisi tunajiuliza ameyapata wapi
amembeba mtoto yule hatujui ni kwa urafiki wake na huyo ama ni urafiki
gani na familia ya huyo mtoto, lakini alimleta shuleni na kumshinikiza
makamu mkuu wa shule amruhusu mtoto arudi shule kusoma lakini tulipopata
taarifa tulijiuliza hii itakuwa ni kinyume na haki na vilevile ni
kudharau bodi ya shule na ofisa elimu hana mamlaka ya kuwarudisha
wanafunzi waliofukuzwa na bodi.
Akizungumzia kitendo hicho mmoja wa walimu shuleni hapo alisema kuwa pamoja na kuendelea na msimamo wa kutoingia madarasani ameutaka uongozi wa juu akiwemo mkuu wa mkoa kuingilia suala hilo kisheria na kuchukua hatua stahiki kwa kulinda maadili ya kazi ya ualimu.
Kwa
mujibu wa malalamiko ya walimu hao ni juu ya ukubwa wa makosa
yanayomkabili mwanafunzi huyo ambaye kwa taratibu hayawezi kuvumilika
katika taasisi yoyote ya elimu nchini kutokana na baadhi ya makosa
kuingilia maslahi na usalama wa familia za jamii inayowazunguka.
Baadhi ya
makosa ambayo mtoto huyo anaidawa kuyafanya ni pamoja na alifumaniwa
mtaani na mume wa mtu kesi yake ikaenda hadi polisi na hapa shuleni ana
kesi ya wizi na kesi ya uzinifu uthibitisho upo na alikiri kwa barua
hayo ni baadhi ya makosa ambayo binti alitenda na bodi iliomba
uthibitisho ofisi ya nidhamu kwa kushirikiana na stafu ya kihesa
ilipeleka viambatanisho bodi na bodi iliridhia kwamba mwanafunzi huyo
kwa viambatanisho kupelekwa pamoja na baba yake mzazi kukiri kwamba
akikamatwa na kosa lingine afukuzwe lakini kinachoshangaza ni kwamba kwa
nini mwanafunzi huyo alifanya makosa kama ya kudhalilisha shule.
Pili mamlaka ya ofisa huyo katika kumrudisha mwanafunzi shuleni hana mamlaka hiyo, alitakiwa kuomba bodi labda aangalie kibinadamu, lakini alishindwa kufanya hivyo ameamua kutumia mamlaka yake kumdhalilisha mkuu wa shule ya kihesa bodi ya kihesa sekondari na walimu wote wa shule hiyo na hatujui ni kwa sababu gani alifanya hivyo na tungependa kujua kwamba anajua mamlaka yake na mipaka yake na sisi tumeasmua hatutaingia madarasani hadi atakapokuja kumchukua mwanafunzi huyo, alihoji.

Tunataka
aje amchukua huyu mtoto pili atuombe radhi sisi walimu wenzake Kwa
sababu anatumia cheo chake vibaya tatu amekurupuka kwa sababu sisi
walimu tuna kazi kubwa kama mbili za kumsaidia mtoto kumlea pamoja na
kumfundisha haiowezekani mtoto kufanya makosa makubwa ya kumfukuzisha
shule tumekaa walimu,bodi ya shule walimu wa nidhamu,kamatiu ya nidhamu
na jopo lote la walimu halafu bodi kumtoa halafu yeye anakuja kumrudisha
hiyo ni kutudhalilisha sisi walimu hatupo tayari kukubali mwanafunzi
aliyefukuzwa na bodi kurudi shuleni.
" Sisi kama walimu hao tumeshikilia msimamo wetu wakidai kudhalilishwa na maamuzi ya kiongozi huyo huku wengine wakijenga hoja juu ya uhalali wa Ofisa huyo kushika madaraka kutokana na rekodi mbaya ya uongozi aliyokuwa nayo tangu awali mwanafunzi huyo ."alisema mmoja wa walimu shuleni hapo.
Kwa upande wa uongozi wa serikali ya wanafunzi dada mkuu wa shule hiyo Neema Mtisi alisema kuwa maamuzi ya bodi yalikuwa sahihi na kwa muda huo kama viongozi walikuwa kwenye pilika za kumwandikia barua mkuu wa mkoa kufikisha kilio cha kukosa masomo kwa siku mbili mfululizo.
Chanzo: MJENGWABLOG

No comments:
Post a Comment