Mama Shujaa wa Chakula 2014 Bahati Muriga akitoa neno la Shukurani
Baada ya Kukabidhiwa zawadi rasmi zawadi zake Wilayani kwake Ukerewe
Eluka Kibona kutoka Oxfam akimkabidhi ufunguo wa Pikipiki Mshindi wa Mama shujaa wa Chakula
Mama Shujaa wa Chakula 2014 Bahati Muriga akisaini kupokea zawadi zake
kutoka OXFAM kupitia Programu ya GROW, Wekeza kwa wakulima wadogo wadogo
Inalipa.
Bwana Hamis Kombo muwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe akitoa salamu
za pongezi kwa Mama Shujaa wa Chakula 2014 pia kuwashukuru OXFAM kwa
kutoa zawadi hizo.
Bahati Muriga akijaribisha kuiwasha Pikipiki yake Mara baada ya Kukabidhiwa
Bahati Muriga akifurahia zawadi zake
Kulwa Kizenga wa kwanza kushoto na Eluka Kibona kutoka OXFAM wakimkabidhi zawadi Bahati Muriga
Mkamiti Mgawe wa kwanza kushoto kutoka OXFAM akiwa na Mama shujaa wa Chakulaa
Zawadi alizopokea Mama Shujaa wa Chakula.
Mshindi wa Maisha Plus/Mama shujaa wa chakula msimu wa tatu 2014 Bahati
Jacob Muriga jana alikabidhiwa zawadi nyumbani kwake Ukerewe. Zawadi
hizo ni vifaa vya kilimo vyenye thamani ya shilingi milioni 20 ambapo
Bahati Muriga alichagua kununua shamba lenye ukubwa wa ekari 7, pikipiki
yenye miguu mitatu aina ya TOYO, vifaa vya kulimo kama vile mbegu,
mbolea, mipira ya kumwagilia, watering cane, water pump, spray pump,
koleo na dawa za kuondoa wadudu na ukungu, majembe, mundu, engine oil
lita 2 na petroli lita 96.
Shindano la Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula 2014 lilifikia tamati
mnamo tar. 18 May, 2014 ambapo Bahati Jacob Muriga ndiye aliyeibuka
kidedea wa shindano hilo. Mama shujaa huyu ni mkulima kutoka Nansio,
Ukerewe mkoa wa Mwanza na pia ni mwalimu mkuu shule ya Msingi Mhozya. Ni
mjane mwenye watoto watatu na hutumia kilimo kama nguzo ya kuhakikisha
mahitaji ya kifamilia yanatimizwa.
Hafla fupi ya kumkabidhi zawadi zake Bahati zilifanyika katika Ukumbi wa
Afro Beach ambapo watu na wawakilishi mbali mbali kutoka serikalini na
mashirika yasiyo ya kiserikali kama vile Kivulini, EMEDO walihudhuria
ili kushuhudia jinsi anavyokabidhiwa zawadi.
Bw. Kombo, akimuwakilisha mkuu wa wilaya ya Ukerewe alionesha furaha
yake kwa mama shujaa kutoka Ukerewe alisema” Ninayo furaha kubwa na kama
kiongozi kijana kuona wilaya yetu imetoa mshindi wa shindano kubwa kama
hili na kuiweka ukerewe katika historia na ramani ya nchi kuwa, kumbe
nasi tunaweza, najisikia furaha pia kwa ushindi huu kwani toka anaanza
huu mchakato wa kuchukua fomu na kuelekea kijiji cha maisha plus nilikua
miongoni mwa niliotoa ushirikiano mkubwa kwa kutoa ruhusa na araka
zangu za yeye kushiriki katika shindano hili kwani ni mwalimu huyu”
No comments:
Post a Comment