Watu
watatu wamekufa, akiwemo mtoto mchanga ambaye mashuhuda wanasema
"alitupwa nje," baada ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace
kurushiwa bomu na watu wasiojulikana huko Kasesema, Kigoma alfajiri ya jana.
Shambulizi
hilo limefanyika jirani na Kambi ya Jeshi ya Migongo wilayani Buhigwe
majira ya saa 11 alfajiri, wakati basi hilo likivusha abiria toka
Kilelema kwenda Kasulu Mjini.
Watu
wengine 6 wamejeruhiwa vibaya katika tukio hilo la kutisha, ameeleza
kamanda wa polisi (OCD) wa wilaya ya Buhigwe, Samuel Utonga.
Mashuhuda
walisema kuwa, wakati Hiace hiyo ilipokuwa ikipita eneo la
Migongo, alijitokeza mtu mwenye bunduki, akasimama katikati ya barabara
akiishinikiza isimame.
Alipoona
dereva hapunguzi mwendo, haramia huyo alilipisha hilo basi, ambalo
lilosonga mbele umbali mfupi tu kabla ya mtu mwingine kujitokeza toka
kusikojulikana na kulirushia bomu.
Taarifa
toka wilayani humo zinasema hali ya wahanga hao wa bomu
"imezidi kuwa mbaya," hivyo imebidi wahamishwe toka hospitali ya Muyama
na kupelekwa Kasulu Mjini kwa tiba zaidi.
No comments:
Post a Comment