WIZARA ya Maliasili na Utalii, imesema
inakabiliwa na upungufu wa askari 3767 wa wanyamapori wanaohitajika
katika kupambana na matukio ya ujangili. (HM)
"Kampeni ya Tokemeza Ujangili, itaanza
kwa awamu ya pili na tumejipanga kuhakikisha hakuna kasoro
zitakazojitokeza. Tunahitaji askari 4855, lakini mpaka sasa tunao askari
1088 ambao hawatoshelezi kuendesha kampeni hiyo," alisema Waziri wa
Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu.
Nyalandu pia amesema askari wote
waliohusika katika hatua ya kwanza ya kampeni ya Tokomeza Ujangili
ambayo ilisimamishwa kutokana na kasoro zilizojitokeza huku wakiwa
hawajapewa haki zao, wanatambulika.
Alikuwa akizungumza na waandishi wa
habari Dar es Salaam jana katika mkutano wa majadiliano na wadau
mbalimbali wa maendeleo uliolenga kutafuta mbinu thabiti ya kupambana na
ujangili.
Nyalandu alisema askari wote watapatiwa haki zao kwa sababu Serikali inawatambua .
"Tunaamini tutapata askari wa kutosha
kwa sababu katika ili hatuko peke yetu bali tunashirikiana na wenzetu
kutoka katika vyombo vya usalama wakiwamo polisi na Jeshi la Wananchi,"
alisema.
Alisema Benki ya Dunia imesema ipo tayari kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania katika kampeni hiyo ya awamu ya pili.
"Nichukue nafasi hii kuwashukuru Benki
ya Dunia kwa kukubali na kuitikia wito uliotolewa na Rais Kikwete
alipowataka wadau wa maendeleo kujitokeza kutusaidia katika kampeni hizi
na wao wameonyesha utayari wao leo," alisema Nyalandu.
No comments:
Post a Comment