MEYA wa Manispaa ya Ilemela kupitia
chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Henry Matata amesema
anatarajia kurejea katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwakani
Amesema atachukua hatua hiyo baada ya kuchoshwa na siasa za unafiki, ubabe, majungu na ukabila ndani ya Chadema.
Akizungumza nyumbani kwake, Matata
alisema anajuta kujiunga na Chadema na kutumia gharama zake kubwa
kukiimarisha na kujikuta akifukuzwa kutokana na majungu.
Matata amewapiga vijembe viongozi
wakuu wa Chadema kuwa wamepoteza uelekeo na wanakiua chama hicho
kutokana na kutokubali ushauri wa kukinusuru chama hicho.
Alisema ameamua kurejea CCM mwaka 2015
kutokana na mazingira yalivyo ndani ya Chadema kwa sasa ambako hakuna
matumaini tena kutokana na mgogoro wa kung'ang;ania madaraka hali ambayo
imekidhohofisha chama hicho.
Matata alisema kabla ya kukimbilia
Chadema alikuwa ndani ya CCM lakini kutokana na kutokutendewa haki
aliamua kukimbia kwa kudhani kile anachokipigania atakwenda kukipata
ndani ya chama hicho lakini hali aliyoikuta kule ni tofauti.
Alisema kwake CCM ni kama nyumbani
ndiyo maana hajuti kurejea mwakani na kuwania nafasi yoyote kutokana na
mazingira yatakavyokuwa kwa wakati huo.
Matata alitamba kuwa anatarajia kuleta
mtikisiko mkubwa ndani ya Chadema mwaka atakapoondoka na idadi kubwa ya
wanachama wakiwamo madiwani ambao wamekuwa wakimuunga mkono. Chanzo:
mtanzania
No comments:
Post a Comment