Mahakama moja mjini Cairo Misri
imeahirisha kesi ya aliyekuwa Rais Mohammed Morsi, baada ya mawakili
wake kuondoka mahakamani kwa hasira.
Mawakili hao wanalalamikia kile
wanachosema ni kuendelea kuzuiliwa kwa Morsi pamoja na waliokuwa
wanachama wa vuguvugu wa Muslim Brotherhood ndani ya chumba cha Glasi
ambacho hakipitishi sauti.
Duru zinasema kuwa mahakama itateua mawakili wengine kumtetea Morsi.
Kesi dhidi ya Morsi itasikilizwa tena Jumapili Ijayo
Rais huyo wa zamani alipinduliwa na
jeshi mwezi Julai baada ya kutuhumiwa kwa kupanga njama na nchi za
Magharibi , utawala wa Pallestina Hamas, kundi la Hezbollah nchini
Lebanon na serikali ya Iran kupanga mashambulizi nchini Iran.
Hii ni moja ya kesi nne zinazomkabili Morsi pamoja na maafisa wakuu wa Muslim Brotherhood.
Iwapo atapatikana na hatia bwana Morsi anakabiliwa na hukumu ya kifo.
CHANZO: BBC
No comments:
Post a Comment