Washika bunduki kutoka jiji la London
maarufu kama ''The Gunners'' wameitandika timu ya Liverpool jumla
ya magoli 2-1 katika mchezo wa kombe la FA na kujihakikishia kutinga
hatua ya robo fainali za kombe hilo, Arsenal ilipigwa jumla ya magoli
5-1 mara ya mwisho ilivyokutana na timu hiyo katika mtanange wa ligi kuu
ya Uingereza; hivyo jana ililipa kisasi na kuwatoa Liverpool katika
kinyang'anyiro cha kombe hilo.
Goli la kwanza la Arsenal lilifungwa
na Oxlade-Chamberlain katika dakika ya 16 ya mwanzo wa mchezowakati goli
la pili likifungwa na Lukas Podolski na baadae timu ya Liverpool
ilipata goli kwa njia ya Penati kupitia kiungo wake Steven Gerrard.
Japokuwa Mwamuzi wa mchezo huo ''
Howard Webb'' ambaye atachezesha baadhi ya michezo ya kombe la dunia
mwaka huu; alionekana tupowapa Liverpool penati ya wazi baada ya
mshambuliaji wake Luis Suarez kuchezewa rafu mbaya ndani ya dimba la
Arsenal na Oxlade-Chamberlain wa timu hiyo.
Arsenal itavaana na timu ya Everton katika hatua ya robo fainal ya kombe hilo la FA.
No comments:
Post a Comment