Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP limetangaza kuwa
Zimbabwe licha ya kukabiliwa na upungufu mkubwa wa bajeti,
inakabiliwa pia na upungufu mkubwa wa chakula na kutishia maisha ya
mamia ya maelfu ya wananchi wa nchi hiyo.
Taarifa iliyotolewa na WFP
imeeleza kuwa, shirika hilo la kimataifa linahitaji dola milioni 90 ili
liweze kuendelea kutoa misaada ya chakula kwa taifa la Zimbabwe katika
kipindi cha miezi sita ijayo.
Imeeleza kuwa, shirika hilo
linahitajia dola milioni 180 ili liweze kutoa misaada yake kikamilifu
kwa nchi za Kusini mwa Afrika kama vile Zimbabwe, Msumbiji, Madagascar
na Jamuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Naye Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano cha WFP mjini Johannesburg nchini Afrika KusiniDavid Orr, amesema kuwa
nchi za ukanda wa Pwani ikiwemo Madagascar zitakabiliwa na baa kubwa la
njaa kabla ya kuanza msimu wa mavuno.
Amesema kuwa, WFP ilishindwa
kutoa misaada kwa wakimbizi wa Kivu Kaskazini nchini Kongo kutokana na
matatizo ya kifedha yanayoikabili taasisi hiyo ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment