Sunday, January 5, 2014

HUU NDIO UJUMBE WA DK SLAA

 Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa ametoa ujumbe ufuatao kupitia mtandao wake wa Kijamii.

Bila watanzania chadema kisingefika hapa ambapo kila mtu anakitambua na watu wengi wanatambua chadema ni chama cha ukombozi wa taifa letu na kila mwanachama anaongozwa na katiba ya chama ndani ya chama kukiwa na viongozi ambao wanasimamia na kuweka sawa mambo mbalimbali ndani ya chama.

Kama katibu mkuu wa chadema nitakuwa mstari wa mbele kusimamia katiba ya chama pamoja na viongozi wangu na kusimamia mtu yoyote ambaye ataenda kinyume na katiba ya chama kwa nia ya kuchafua chama chetu hatutaweza kuangalia jina la mtu wala sura ya mtu bali tutasimamia katiba ya chama.

Watu ambao wapo chadema kwa nia ya kukichafua chama ni bora kuondoka mapema kuliko kuja kuumbuka na kama upo chadema kwa nia nzuri ya kujenga harakati za uzalendo ndani ya taifa lako basi Tuwe pamoja katika mapambano ya kujenga chama pamoja na taifa letu.

Watanzania ambao mnakipenda chadema kama chama napenda kuwaeleza kuwa kuweni makini hasa kipindi hiki ambacho watu wanaingia ili kuweza kuvuruga mapambano kwa rushwa mbalimbali uweze kufanya mambo yoyote ili chadema kiweze kuonekana ni chama kibovu wakati kinasimamia maamuzi yake ndani ya chama.
 

No comments:

Zilizosomwa zaidi