Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto
Kabwe, amejibu mashambulizi kwa viongozi wa Chadema, kutokana na kile
alichosema wanazunguka na kusema maneno yasiyo ya ukweli.
Akihutubia maelfu ya wananchi
waliokusanyika katika Uwanja wa Mwanga Centre, Kigoma mjini, alisema
alichukua kadi ya uanachama wa Chadema mwaka 1993 wakati huo, Katibu
Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa akiwa bado yuko CCM.
"Wakati hao wenye midomo mikubwa
wanaoongea sasa, walipokuwa wamekumbatia watawala, nyinyi mlikuwa
mnapigwa mabomu kutaka mageuzi, eti leo wao wapinzani zaidi kuliko sisi
na ndiyo maana hatuwezi kuwaachia.
Hatuwezi kukubali, hatutoki,
demokrasia ni mchakato na mwenzenu nimekuwa kwenye mchakato huu. Kadi
yangu ya Chadema nimeichukulia kwenye uwanja huu, tarehe moja mwezi wa
nne mwaka 1993, nikiwa na miaka 16, wakati nachukua kadi yangu, Katibu
Mkuu wa chama changu alikuwa yuko CCM.
Akizungumza kile alichosema ni uongo
unaosambazwa na viongozi wa juu wa chama hicho, Katibu Mkuu Dk Slaa na
Mwenyekiti wake Mbowe waligawana maeneo Mbowe akaenda Kanda ya Ziwa na
Dk Slaa Kanda ya Magharibi.
Alisema kwenye mikutano hiyo, Mbowe
anasema kuwa endapo mbunge huyo atarudi yeye Mbowe atajiuzulu, suala
alilosema linaonyesha kuwa tayari ameshafukuzwa bila hata utetezi wake
kusikilizwa.
Alisema baada ya viongozi hao
kuzungumza na kusema mambo hayo na yeye aliamua kurudi nyumbani Kigoma
na baada ya kuona hilo Dk Slaa akahoji mbunge huyo anafanya vikao hivyo
kama nani.
"Mimi nimekata rufaa, wajumbe wa
baraza kuu wa Mtwara, Ruvuma wanaandika barua wanataka mkutano mkuu,
Katibu Mkuu akiwa Igunga anasema hiyo ni haramu na hao wafuasi wa Zitto
watafanya Zitto afukuzwe''
No comments:
Post a Comment