Sunday, November 3, 2013

DR. SENGONDO MVUNGI AVAMIWA NA KUJERUHIWA VIBAYA KWA MAPANGA USIKU WA KUAMKIA LEO JIJINI DAR

Dr Sengondo Mvungi
Dr Sengondo Mvungi mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha upinzani NCCR-Mageuzi ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya  Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchi na mhadhiri mwandamzi wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Bagamayo amevamiwa na kujeruhiwa vibaya usiku wa kuamkia leo. 

Imeelezwa kuwa, saa saba usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Dr Mvungi alivamiwa na watu wasiyojulikana na kumacharanga mapanga maeneo ya mwilini mwake ikiwemo sehemu za kichwani.

Inadaiwa kuwa watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walikuwa wakimshinikiza awapatie fedha na Dk.Mvungi alipowaambia hana fedha ndipo walipoanza kumcharanga mapanga.

Mtoto mkubwa wa Dk.Mvungi, Dk.Natujwa Mvungi ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Bagamoyo Dar es Salaam,alieleza kuwa mnamo saa nane usiku ndipo walipovamiwa na kumjeruhi vibaya baba yake.

Dk.Natujwa anasema baada ya watu hao kumjeruhi baba yake na kufanikiwa kuondoka, walimchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Tumbi mkoani Pwani, na kupatiwa matibabu ya huduma ya kwanza na kasha walimpeleka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alipokelewa Emergence na kisha saa kumi na moja asubuhi aliingizwa kwenye wodi ya Taasisi ya Mifupa Moi kwaajili ya kuanza kupewa matibabu.

No comments:

Zilizosomwa zaidi