Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Kishepu Ndugu Isabela Chilumba wakati wa mapokezi yake katika kata
ya Isaka.
Wakazi wa Isaka wakiwasikiliza viongozi wa CCM Taifa waliowasili mkoani Shinyanga leo kwa ziara ya siku nne.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Isaka na kuwaambia
muda wa kudanganyika na wanasiasa uchwara umefikia kikomo.
Mwanachama wa CCM akifurahia hotuba ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Isaka.
Mbunge wa Msalala Ndugu Ezekiel Maige akizungumza na wakazi wa Isaka wakati wa mkutano wa hadhara .
Wana CCM wa
Isaka wakishangilia hotuba ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Ndugu
Hamisi Mgeja kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Isaka .
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kufyatua matofali ya ujenzi wa
tanki la maji katika kijiji cha Kagongwa kata ya Kagongwa.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na wananchi wa kijiji cha
Mwendakulima baada ya kuzindua awamu ya kwanza ya ujenzi wa kituo cha
afya kilichodhaminiwa na kampuni ya uchimbaji wa madini ya Africa
Barrick Gold.
Katibu Mkuu
akishiriki kupanda mti katika kituo cha afya kilichodhaminiwa na mgodi
wa Buzwagi chini ya kampuni ya Africa Barrick Gold .
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimwagia maji mti alioupanda kwenye kituo cha afya katika kijiji cha Mwendakulima.
Katibu Mkuu wa CCM akishiriki kupiga lipu ofisi ya kata ya Majengo katika wilaya ya Kahama.
Katibu
Mkuu wa CCM akifungua SACCOS ya Mkombozi ya vijana wa CCm mjini Kahama
ambapo aliwezesha kutatua masuala yote ya msingi yanayowakabili vijana
hapo, hasa yanayohusu elimu ya uraia , uchumi ,elimu za ufundi ambapo
vijana kumi watapata nafasi ya kulipiwa na Katibu Mkuu na masuala ya
maeneo ya kufanya shughuli za biashara.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdul Rahman Kinana akiingia ukumbini kwa ajili ya kufanya
mkutano na mabalozi wa nyumba kumi kwenye ukumbi wa Halmashauri ya
Kahama.
Katibu wa NEC Nape Nnauye akiingia kwenye uwanja wa CDT tayari kwa kuhutubia mkutano wa hadhara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye kiwanja cha CDT kwa ajili ya kutubia wakazi wa Kahama.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana akiwapongeza wacheza sarakasi waliokuja kumsabahi kwa staili ya kipekee kabisa.
Sehemu ya Umati
uliofurika kusikiliza hotuba za viongozi mahiri wa CCM, Katibu Mkuu
Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
leo kwenye viwanja vya CDT mjini Kahama.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kahama wakati mkutano wa hadhara uliofanika leo mjini Kahama.
Katibu Mkuu Ndugu
Abdulrahman Kinana akipokea kadi kutoka vyama vya upinzani baada ya
wananchi wengi kuridhika na hotuba yake nzuri, katika mkutano huo zaidi
ya wanachama 560 wamejiunga na CCM kutoka vyama vya upinzani.
No comments:
Post a Comment