Friday, September 20, 2013

MASOGANGE NA MELISA WAACHIWA HURU KWA SH. MILIONI 4.8

Agnes Gerald (Masogange)
Agness Gerard ‘Masogange’ na Melissa Edward wameachiwa huru na Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg baada ya kutakiwa kulipa faini ya Sh 4.8 milioni (Randi 30,000) kwa kosa la kubeba kemikali zinazotumiwa kutengeneza dawa za kulevya.
Msemaji wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai cha Afrika Kusini (hawk) Kapteni Paul Ramaloko alisema Watanzania hao wameachiwa huru baada ya kuonekana kuwa hawakubeba dawa za kulevya bali kemikali aina ya ephedrine.
Hata hivyo mahakama ilibaini kuwa Melissa hana hatia kwa kuwa ilionekana amemsindikiza Masogange, aliyemuomba amsaidie kubeba mzigo huo.
Mosagange alilipa faini ya Shilingi 2.5 milioni (R15, 000), huku akiahidi kumaliza nusu yake ambayo juhudi zilikuwa zinafanyika amalize kulipa jana Ijumaa.
“Mahakama iliona kuwa Melissa aliombwa tu kusaidia kubeba baadhi ya mabegi, lakini haikuwa mizigo yake. Mizigo yote iliandikwa jina la Agness Masogange na si Melissa,” alisema Kapteni Ramaloko.
Kapteni Ramaloko alisema, Melissa alijitetea kuwa hakuwa amesafiri na Masogange bali walikutana ndani ya ndege na Masogange alimuomba amsaidie mizigo hiyo kwani ilikuwa mikubwa.
Kwa sheria za Afrika Kusini kubeba kemikali zozote ambazo zimepigwa marufuku ni kosa la jinai kisheria hivyo mahakama iliamuru Masogange ahukumiwe kwenda jela miezi 30 (miaka miwili na miezi sita) au alipe faini ya R30, 000(Sh 4.8 milioni).
Hata hivyo alilipa faini na nusu ya fedha hizo ilishalipwa na nyingine ilikuwa inakaribia kulipwa.
Ingawa Kamishana Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa alipoulizwa juzi Alhamisi alisema mzigo walioubeba Masogange na mwenzake haukuwa ni dawa za kulevya bali ni kemikali za dawa za kulevya, lakini Msemaji wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini, (SARS) Marika Muller, alieleza kuwa timu ya SARS ina uhakika kuwa mabegi sita yaliyokamatwa Julai 5, mwaka huu ni methamphetamine.

No comments:

Zilizosomwa zaidi