Friday, September 13, 2013

HABARI YA PADRI KUMWAGIWA 'TINDIKALI' HUKO ZANZIBAR HII HAPA

Padri Anselmo Mwang'amba baada ya tukio la kumwagiwa tindikali.
Padri Anselmo Joseph Mwang'amba wa Kanisa Katoliki Parokia ya Cheju, mkoa wa mjini magharibi visiwani Zanzibar anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 50, amemwagiwa maji yanayodhaniwa kuwa ni tindikali alpoikuwa internet cafĂ© majira ya saa tisa alasiri maeneno ya Mlandege.

Kwa mujibu wa kamanda wa Jeshi la Polisi mjini Magharibi, Mkaadanu Hassan Mkaadanu, Padri huyo alipigiwa simu, na alipokuwa akitoka nje ili kuisikiliza vema simu, hapo ndipo tukio likatokea, ambao haijajulikana kama ni mtu au kundi la watu lililofanya tukio hilo.

Taarifa za hivi sasa zinaeleza kuwa Padri Mwang'amba amelazwa Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja, wodi ya Mapinduzi mpya, ambayo ni wodi maalum kwa ajili ya viongozi.

Padri huyo amefanya kazi kwa muda wa zaidi ya miaka 35 huko Zanzibar, ambapo baada ya taarifa hizi kupatikana, askofu mkuu wa kanisa katoliki Zanzibar, Agustino Shao ameelezwa kujifungia kuanzia muda huo na kuendelea kuwepo hadi muda huu

Kwa hivi sasa taharuki ni kila mahali, hakuna kinachoeleweka, wakristo wakieleza kuwa hawana pa kukimbilia kwa kuwa ni zaidi ya miezi minne kupita tangu Padre Everist Mushi auawe na bado mwenendo wa kesi haueleweki, na kwamba sasa hawajui pa kwenda.

Kamanda Mkaadamu amekiri kuwa tindikali ni tatizo, na amesema kuwa wanaendelea kufanya jitihada ili kila kitu kiwe wazi.

No comments: