Monday, September 23, 2013

AJARI MBAYA YAUA ASKARI WATATU WA OPARESHENI KIMBUNGA

Askari Polisi watatu wa operesheni Kimbunga ya kusafisha wahamiaji haramu nchini, wamefariki dunia jioni ya jana mjini Kahama kufutia ajali ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Muleba mkoani Kagera kuelekea makambako mkoani Njombe. 

Marehemu hao waliotambulika kwa majina ya Kopolo Fred,PC Subian na PC Michael wote ni askari wa kituo cha Polisi Makambako, na mauti yamewafika baada ya gari nambari PT 0776 Land Rover Diffender kuacha njia na kupinduka. 


Ajali hiyo imetokea katika eneo la Sungamile Kata ya Kagongwa wilayani Kahama wakati dereva wa gari hilo PF3270 PC Yusuph, akijaribu kumkwepa Bibi Kizee mmoja huku gari likiwa kwenye mwendo kasi hali iliyosababisha kumshinda na kupinduka.

Kumbukumbu za kipolisi zimeonesha kuwa hapo jana jioni askari wengine walipata ajali katika kijiji cha Igusule wilayani nzega ambapo askari 4 wamelazwa katika hospitali ya wilaya Kahama huku mmoja akiwa na hali mbaya. 

Oparesheni Kimbuga ni utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete, la kuwaondoa wahamiaji haramu nchini, ambapo vikosi vya ulinzi kwa pamoja viliunda kikosi kimoja na kufanya kazi nchini kote.

No comments:

Zilizosomwa zaidi