Monday, August 26, 2013

STENDI YA DALADALA DODOMA YAKAMILIKA NA KUANZA KUTUMIKA HUKU MACHINGA WAKIZUIWA KUJENGA VIBANDA..

 Abiria wakiwa tayali wameshuka katika Daladala baada ya kutoka maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma na kushushiwa Barabarani baada ya kukuta msongamano mkubwa katika stand mpya iliyoanza kutumika leo ya jamatini.

 Mmoja wa viongozi wa wafanyabiashara Ndogondogo Danny Msitewa akifafanua jambo alipokuwa akisoma majina na kuwapa namba za utamburisho wa nafasi za kuweka vibanda vyao katika stand mpya ya Daladala ya Jamatini Dodoma
 Wafanya biashara waliokuwa stend iliyokuwa ya muda ya daladala oil com wakikusanya bidhaa zao zilizosambazwa na tingatinga lililofika kubomoa vibanda walivyokuwa wakaifaanyia biashara zao ili kuwashinikiza kuondoka eneo hilo.
 Asikari akitoa maelekezo kwa baadhi ya watu waliokuwa wakivizia kukwapua mali za watu zilizozagaa stand ya Daladala ya oil com Baada ya kubomolewa vibanda vyao ili wahame katika eneo hilo.
 Mwenyekiti wa Mipango miji na Mazingira manispaa ya Dodoma Stephen Mwanga akiwatangazia wafanya biashara ndogondpgo kutoendelea na ujenzi mpaka baazi ya taratibu zitakapokamilishwa.
 Msukuma Tololi akiingiza moja ya vibanda vya wafanyabiashara katika Stand mpya ya Daladala ya Jamatini Dodoma iliyoanza kutumika leo 
 Magali ya Daladala yakisubili abiria  ndani ya Stand Mpya ya Jamtini Dodoma iliyoaanza kutumia leo huku kukiwa nachangamoto ya wingi wa magali hayo kiasi cha kushia abiria barabarani kutokana na ufinyu wa stand hiyo.
 Daladala zikisubili kuingia ndani ya Stand Mpya ya Jamtini Dodoma iliyoaanza kutumia leo huku kukiwa nachangamoto ya wingi wa magali hayo kiasi cha kushia abiria barabarani kutokana na ufinyu wa stand hiyo. 
 Kazi ya bomoa bomoa ikiendelea stend ya mkoa

MWENYEKITI wa kamati ya Mipango miji na Mazingira Manisipaa ya Dodoma Stephen Mwanga Amesimamisha ujenzi wa vibanda vya wafanya Biashara ndogondogo [machinga] katika stend ya Daladala ya Jamatini baada ya kutolidhishwa na Ugawaji wa nafasi zao.
Machinga hao wamesimamishwa kujenga siku ya kwanza tangu stend hiyo kuanza kutumika baada ya kufungwa mwaka mmoja uliopita ili kupisha ujenzi utakaokidhi haja ya watumiaji wa magali hayo yanayotoa huduma za usafiri wa ndani ya mji wa Dodoma.

Mwenyekiti huyo amewataka kusimamisha zoezi hilo la ujengaji wa vibanda vya biashara zao kutokana na kile alichosema  ugawaji wa nafasi hauzingitia utarabu kutokana na viongozi wa machinga hao kupewa jukumu la kusimamia.

Mwanga aliongeza kuwa alifika eneo hilo kutokana na kusikia malalamiko ya baadhi ya machinga kulalakia kutotendewa haki wakati zoezi la ugawaji likiendelea kwakuwa wengi wao walijikuta wakiwekwa pembeni tofauti na walipokuwa kabla ujenzi huo haujaanza Augost 2012.

Baada ya kufika na kujionea kilichokuwa kikiendelea Stend hapo aliamua kumjulisha mkurugenzi hali halisi na hivyo kuamuliwa zoezi la ujenzi na uwekaji wa vibanda lisimamishwe na kamati ndogo iundwe ili ikutane na uongozi wa manispaa ili walijadili na kuliweka sawa swala hilo.

'' Nimesimamisha ujezi usiendelee kwa sababu mtu akishajenga kumuondoa inakuwa ngumu, mimi na kamati yangu ya mipango miji na mazingira tutakutana na Meya na Mkurugenzi wa manispaa ili tulitatue swala hili kwa pamoja na kamati yao mapema
iwezekanavyo ili Abiria waendele kupata mahitaji yao kama kawaida'', alisema Mwanga

kwa upande wao baadhi ya Machinga hao walisema viongozi wamejilimbikizia nafasi zaidi ya moja kwa kutumia majina tofauti mpaka ya wake zao huku sura nyingi mpya zikipenyezwa hata wakati stend hiyo kabla ya kuhamishwa hawakuwepo huku nafasi hizo zikibanwa kuwa ndogo na wao kujipendelea nafasi za mwanzo.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara hao wadogo wadogo Haji kulaya alisema mpangilio huo wa viongozi hauwezi kubadilishwa kutokana na ramani ya stand hiyo kubadilika kuwa tofauti na ilivyokuwa mwanzo hali iliyofanya kuwe na mpangilio mpya katika ugawaji.

No comments:

Zilizosomwa zaidi