Sunday, August 25, 2013

SOLDADO AANZA MSIMU KWA KASI...


Roberto Soldado

Mshambuliaji mpya wa Tottenham Spurs Roberto Soldado ameanza vema kibarua chake katika timu hiyo kwa kuonyesha umahili wake wa kutikisa nyavu akiwa ameeshafunga mabao manne katika michezo mitatu aliyoichezea Tottenham. Soldado amefunga goli lake la  nne leo likiwa ni goli pekee lililoipa ushindi Tottenham dhidi ya Swansea.
Wiki iliyopita wakati wa ufunguzi wa msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya Crystal Palace, Soldado alifunga goli pekee kwa mkwaju wa penalty ambalo pia  liliipa ushindi timu yake. 
Soldado amesajiliwa akitokea Valencia kwa uhamisho wa ada ya 30 million euros ($40 million).
Magoli ya Soldado yanatoa hofu kwa Tottenham juu ya kumkosa mshambuliaji wake Gareth Bale anayehofiwa kutaka kutimkia Real Madrid.
By: Mligo G

No comments:

Zilizosomwa zaidi