Sunday, August 11, 2013

JK ATAKIWA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA VYOMBO VYA DOLA...

Chama cha wananchi CUF kimemuomba rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kuchukua hatua juu ya vyombo vya dola vinavyoendeleza tabia ya kutumia vyombo vya moto kukabiliana na raia na kusababisha majeraha na hata kupelekea mauaji ya raia kwa kigezo cha kulinda amani.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la kupigwa risasi kwa sheikh Ponda Issa Ponda huko mjini Morogoro .
Aidha Profesa Lipumba amesema amefanikiwa kwenda kumuona katika hospital ya taifa Muhimbili na kusema amepigwa risasi bega la kulia.
Chanzo ITV

No comments: