Siku kadhaa baada ya
klabu yake ya
Simba kutangaza
kumtema mchezaji wao
mkongwe Juma Kaseja,
mkongwe Juma Kaseja,
hapo jna kocha wa timu
wa timu ya taifa ya
Tanzania Mdenmark
Kim Poulsen
ametangaza kikosi cha
timu ya taifa na
kumjumisha Kaseja
ndani ya kikosi hicho.
Poulsen
akiongea nawaandishi wa habari
wakati akitangaza
kikosi hicho kinachojiandaa na michuano ya CHAN na kiporo
cha mechi ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Gambia,
alisema amekuwa akisoma na kusoma sana habari zinamhusu
Kaseja na klabu yake kupitia kwenye vyombo
vya habari, lakini yeye kwa upande wake amesema bado
anamuamini Kaseja na ataendelea kuwa mchezaji muhimu
ndani ya kikosi chake.
"Nimekuwa nikisikia taarifa nyingi zinamhusu nahodha wetu
Juma Kaseja, ningependa kuweka suala hili wazi kwamba Kaseja
bado ni mchezaji mzuri na anafanya kazi nzuri sana ndani ya
timu ya taifa. Ni nahodha mzuri kwa sababu ni kiongozi mzuri
kwa wenzie nje na ndani ya uwanja. Hivyo kwangu hali
itaendelea kuwa vile vile na nategemea kesho kumuona
akijiunga na kambi ya timu ya taifa, ataendelea kuwa nahodha
na pia golikipa namba 1 wa kikosi changu. Kuhusu yeye na klabu
yake nisingependa kuyaingilia, lakini kwangu Kaseja bado ni muhimu
kwa sababu amekuwa akifanya nzuri kwenye timu ya taifa.
Kuhusu hatma ya huko mbele, tusubiri muda utaongea," alisema
Kim Poulsen.
Wachezaji wengine walioitwa kwenye timu ya Taifa ni hawa hapa,
Kwa Makipa- Ally Mustapha, Mwadini Ally, Aishi Mwanula.
Mabeki: Aggrey Morris, Kevin Yondani, Canavaro, Shoamari
Kapombe, Erasto, Vicent, David Luhende
Viungo: Mcha Khamis, Kazimoto, Sure Boy, Domayo,
Chanongo, Kiemba
Washambuliaji: Mrisho Ngassa, Simon Msuva, John Bocco, Juma
No comments:
Post a Comment