Leo ni ufunguzi wa rasimu ya katiba
mpya na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba
amesema kwamba Rasimu hiyo imependekeza kwamba
matokeo ya rais yahojiwe mahakamani.
Kwa lugha nyingine ni kwamba katiba ijayo itaruhusu Rais
kushtakiwa mahakamani endapo matokeo yake yatatiliwa shaka na wagombea
wengine.
Jaji Warioba ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa
Rasimu ya Katiba Mpya katika tukio la kihistoria nchini Tanzania.
"Imependekezwa kwamba matokeo ya Rais yatashikiwa mahakamani lakini kwa masharti," amesema Jaji Warioba hivi punde.
Jaji Warioba ametaja masharti hayo ni kwamba wagombea wa
urais ndio watakuwa na haki ya kuhoji matokeo ya rais na si vinginevyo.
Pili, matokeo hayo yanatakiwa kuhojiwa ndani ya mwezi mmoja tu na si
vinginevyo.
Amesema pia tume imependekeza kuwapo kwa wabunge wa aina
mbili ambao ni wabunge wa kuchaguliwa na wabunge wengine wa kuteuliwa na Rais.
Pia amesema kwamba kutakuwapo kwa utaratibu wa wanawake kugombea
katika majimbo. Kwa maana hiyo hakutakuwapo wabunge wa Viti Maalumu.
Pamoja na hayo, tume ya jaji Warioba
imependekeza kuwepo kwa serikali tatu ambazo ni -serkali ya
zanzibar, ya tanganyika na ya muungano.
mambo ya muungano yaliyopendekezwa:
1)katiba ya jamhuri ya muugano wa tanzaia
2)sarafu na benki kuu
3)mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa
4)ushuru
5)ulinzi na usalama
6)usajili wa vyama vya siasa
7)uraia na uhamiaji
No comments:
Post a Comment