(Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi) |
Wakati leo ni Siku ya Fistula duniani
huku hafla ya kitaifa ikifanyika jijini Dar es Salaam Makao Makuu ya
CCBRT, wakazi wa Morogoro wametaka kampeni ya fistula kusambazwa
vijijini ili kutoa somo kwa wanawake wengi wenye matatizo hayo.
Fistula ni ugonjwa unawapata wanawake wengi kwa
kutokwa na haja zote kwa wakati mmoja bila kujitambua. Kampeni ya
kuelimisha umma kuhusu fistula ilyoanzia mkoani Kagera imeingia mkoani
Morogoro ikiwa ni kampeni ya kuelimisha umma kuhusu fistula.
Wamesema ingawa walikuwa wakifahamu kuhusu tatizo
la fistula, lakini elimu hiyo iliyohusisha ushuhuda kutoka kwa baadhi ya
wanawake waliowahi kukumbwa na fistula na baadaye kupata matibabu
imewapa uelewa na ufahamu mpana zaidi ambao ipo haja ya kuhakikisha
ujumbe huo unafika kila kona ya nchi hususan vijini.
“Nimefurahi sana nimeelimika vya kutosha kuhusu
fistula. Mwanzoni nilifika hapa kumshuhudia Msanii Mwana FA lakini
mawazo yangu yalibadilika ghafla na kujikuta naguswa na elimu ya
fistula.”alisema Emmanuel Nyangaka.
Kwa upande wake pamoja na kupongeza juhudi za
Vodacom pamoja na kuuliza maswali kadhaa, mkazi mwingine Hassan Ndungate
alisema elimu hiyo ni fusra ya kipekee kwa jamii kujua mambo mbalimbali
yanayohusu fistula ili waweze kutoa msaada au na kuhamamisha jamii
kujitokeza kupata matibabu.
Alishauri elimu hiyo iendelee hadi vijiji mbalimbali.
No comments:
Post a Comment