(Pichani
ndio matundu ya risasi tatu zilivyorindima kwenye kioo cha dereva na kumjeruhi dereva sehemu ya bega na kufanikiwa
kunyakua begi linalosadikiwa kuwa,lilikuwa na kiasi cha fedha shilingi
milioni 40 na kutokomea nazo.)
Ambapo
kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio wanaeleza kuwa
majambazi hao walikuwa wapatao wanne wakiwa wamepanda piki piki,ghafla
wakasimama na kulizunguka gari aina Vitz yenye usajili wa namba T929
CCX (pichani chini) kwa haraka,mmoja wao akiwa na mashine gun na
wengine walikuwa na bastola.
Mmoja
wao alifyatua risasi hewani kumtaka dereva asimame na ashushe vioo vya
gari yake,kufuatia hali ya utata wa majibishano ya muda mfupi
majambazi hao waliifyatulia risasi kadhaa gari hiyo upande wa dereva,
bahati mbaya wakamjeruhi sehemu ya bega,ndipo wakafanikiwa kuondoka na
begi kubwa linalosadikiwa kuwa lilikuwa na kiasi cha fedha shilingi
milioni 40 (kwa mujibu wa dereva aliempeleka majeruhi hospitali).
Mara baada ya majambazi hayo kutimka wasamalia wema wakamchukua dereva huyo aliyekuwa akigugumia kwa maumivu ya jeraha lake na kumtafutia tax na hatimae kumkimbiza hospitali ya Kairuki kwa huduma ya haraka.
Mara baada ya majambazi hayo kutimka wasamalia wema wakamchukua dereva huyo aliyekuwa akigugumia kwa maumivu ya jeraha lake na kumtafutia tax na hatimae kumkimbiza hospitali ya Kairuki kwa huduma ya haraka.
Baadhi ya watu wakijaribu kubadilshana mawazo kwa kulitafakari tukio hilo la ujambazi.
Gari iliyokuwa imevamiwa na majambazi ikikokotwa na gari la polisi mara baada ya kushindwa kuwaka.
No comments:
Post a Comment