Tuesday, March 26, 2013

ZITTO KABWE AMALIZA MAFUNZO YA JKT HUKO TANGA...!




Mbunge wa Kigoma CHADEMA, Zitto 
Kabwe pamoja na Wabunge wenzake 
kadhaa vijana leo wakemaliza rasmi
mafunzo yao ya awali ya JKT katika 
kambi ya Mgambo 835KJ kilichopo
Mkoani Tanga.



Pichani juu ni Zitto Kabwe akijiandaa kwenda katika
gwaride la mwisho na picha chini akiwa shambani
pamoja na Mbunge mwenzake  Iddi Azan, Abdallah 
haji, Raya Ibrahim na Antony Mbassa kambi ya 
Mgambo 835KJ.

Aidha Zitto Kabwe amesema anafuraha iliyo pitiliza 
kumaliza mafunzo hayo na ameweka historia ya 
kubwa katika maisha yake hii leo. Anapasha zaidi 
katika wakati wa Zoezi la kulenga shabaha alifanikiwa
kulenga risasi 3 akiwa amelala, 3 akiwa amepiga 
magoti na 1 akiwa amesimama.

No comments:

Zilizosomwa zaidi