Monday, March 18, 2013

WASIOKUWA NA TAALUMA WABAINIKA KUUZA DAWA MUHIMU.

Watu 462 kati ya 1,205 mkoani Mwanza waliokuwa wakisailiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia Baraza la Famasi, wamebainika kuwa na vyeti bandia.
Kubainika huko kulijitokeza wakati wakifanyiwa mafunzo kuhusu uuzaji wa dawa katika maduka muhimu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Mwanza, Mratibu wa Mpango wa Maduka Muhimu katika Baraza la Wafamasi, Richard Silumbe, alisema Mkoa wa Mwanza, umeongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu waliobainika kuwa na vyeti bandia.
Kwa mujibu wa mratibu huyo, tatizo lilibainika wakati wa kutoa mafunzo elekezi kwa wanafanya kazi wa maduka ya dawa baridi, katika mikoa mbalimbali nchini.

“Asilimia 46 ya waliofika katika usaili huo, walikuwa na vyeti bandia kutoka katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando na vingine vikitoka katika Chuo cha Kanisa la AIC Korandoto. Hali hii imetutisha kwa sababu watu hawa wapo madukani na wanawahudumia wananchi,” alisema Kilumbe.

Alisema pamoja na kuwachuja wauguzi hao waliokuwa wameomba kupata mafunzo ya uuzaji wa maduka ya dawa muhimu, bado kuna wengine waliobainika kuwa hawana ujuzi wowote katika fani hiyo.

No comments:

Zilizosomwa zaidi