Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeongeza siku mbili za kupiga kura
ya kuchagua wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, zoezi ambalo awali
lilipangwa mara ya kwanza kufanyika kati ya Machi 30 mpaka Aprili 3,
mwaka huu.
Mabadiliko hayo ya ratiba yamekuja baada ya
baadhi ya makanisa kutumia ibada ya juzi Jumapili pamoja na mambo
mengine kuonya juu ya ratiba hiyo ya Tume kuwanyima haki wafuasi wa dini
ya Kikristo kutokana na siku zilizokuwa zimepangwa kuangukia kwenye
Sikukuu ya Pasaka.
Katibu wa Tume hiyo, Assaa Ahmad Rashid aliieleza Mwananchi jana kuwa muda umesogezwa mpaka Aprili 5 mwaka huu badala ya Aprili 3 kama ilivyokuwa imetangazwa awali.
“Kwa mujibu wa mabadiliko mapya, vikao hivyo sasa vitafanyika kati ya Machi 30 hadi Aprili 5, kwa msingi huu kila kijiji au mtaa kitachagua tarehe ambayo wananchi watapiga kura kuwachagua wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya,” alisema.
No comments:
Post a Comment