Saturday, March 16, 2013

UPENDO KILAHIRO AFUNGUKA KUHUSU BIASHARA YA NYIMBO MTANDAONI.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini, Upendo Kilahiro amewataka wamiliki wa kampuni za kuuza kazi za wasanii mitandaoni, kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa wasanii ili kuweka uwazi katika biashara hiyo.
Upendo alisema kwamba wasanii wengi hawana uelewa katika matumizi ya mtandao, hivyo bado kuwa gizani kuhusu umiliki wa kazi zao zilizopo katika mtandao na namna zitakavyowalipa.
"Sisi tunaimba muziki wa Injili, baadhi yetu tunajua matumizi ya mtandao na wapo wasiojua, tunawasaidia vipi hawa? Pia muziki wa kizazi kipya na taarabu ni hivyo hivyo, nadhani elimu inahitajika zaidi ili msanii aweze kujua haki yake kikamilifu,"
"Licha ya kuwepo hilo, bado hakuna uwazi ni namna kazi zetu zitauzwa, nadhani wapo wengi wanaojiuliza hili. Uwazi unahitajika zaidi ili kuwa na amani kati ya sisi na wamiliki wa mtandao husika."

No comments:

Zilizosomwa zaidi