Thursday, March 28, 2013

MAAMBUKIZI YA VVU, YAPUNGUA NCHINI..

Serikali imesema kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi Tanzania imepungua kwa asilimia 5.1 huku Wanawake wakiwa hatarini zaidi kupata maambukizi hayo kwa kuwa na asilimia 6.2 ikilinganishwa na Wanaume wenye asilimia 3.8

Raisi Jakaya Kikwete amesema pamoja na ripoti hiyo kuonyesha kupungua kwa kasi ya maambukizi ya VVU, Mkoa mpya wa Njombe unaongoza kwa kuwa na asilimia 14 ukifuatiwa na Iringa wenye asilimia 9.1 ya maambukizi.

Kutokana na ripoti ya utafiti wa viashiria vya ugonjwa wa Ukimwi pamoja na Malaria Tanzania uliofanywa kwa mwaka 2011/2012 na ripoti kuzinduliwa na Rais Kikwete Dar es salaam, kupungua kwa kasi ya maambukizi kumetokana na hamasa kubwa ya Wananchi kujitokeza kupima afya zao ambapo hadi sasa zaidi ya Watanzania milioni 18 wamepima afya zao huku Wanawake ndio wakiwa wamejitokeza kwa wingi kuliko wanaume.

No comments:

Zilizosomwa zaidi