JESHI LA UFARANSA LATUA MALI DHIDI YA WAPIGANAJI WA KIISLAM .....
Wakatia mapigano yakiendelea nchini Mali, Jeshi la Ufaransa limetuma ndege nyingine kwenda kuteka miji mingine nchini mali. Tayari mji wa Diabaly, ambao uko umbali wa kilomita 400 kutoka mji mkuu, Bamako,
umetekwa katika makabiliano yaliyofanyika kati ya waasi na wanajeshi.
Wanajeshi wa Ufaransa wanatumia ndege kuendelea kuwashambulia wapiganaji
wa Kiislamu nchini Mali na wametuma kikosi kwenda kulinda mji mkuu wa
Mali, Bamako.
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, alisema wanajeshi
wamewashambulia wapiganaji waliokuwa wakielekea mji wa Mopti.
No comments:
Post a Comment