Monday, June 15, 2015

TOFAUTI YA WABUNGE WA TANZANIA BARA NA VISIWANI IKO HAPA


Hayo mabasi hapo yametolewa bure kabisa na mbunge wa eneo la Bububu, huku unguja wanamwita Mwakilishi na anajulikana kwa jina la BHAA.
Magari haya ni kwa ajiri ya kuwabeba wanafunzi tu. Hii ilikuja mara tu baada ya kuona adha na changamoto wanayoipata wanafunzi likifika swala zima la usafiri.
Sasa hii inaonesha wazi kuwa wale wabunge wa Tanzania Bara  wao hawawazi hata kidogo ila utawasikia wakisema 'Serikali inajipanga kutatua tatizo la usafiri kwa wanafunzi"
Maana yake wao hii haimo akilini mwao hata kidogo.
Yani hii ni sawa na kusema kuwa tumewapa dhamana ili wale na kujineemesha wao bila kuchukua hatua kwa baadhi ya matatizo yanayowakabiri raia..
Hii ni kwa swala hilo tu ila yapo mengi

No comments:

Zilizosomwa zaidi