Monday, September 8, 2014

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAUNDA KIKOSI KAZI KUTOKOMEZA UJANGILI



Wizara ya Maliasili na Utalii inatarajia kuunda kikosi kazi kwa kushirikisha Wizara ya Mambo ya ndani, na Wizara ya uchukuzi ili kuweza kufanya kazi kwa pamoja kwa nia ya kuweza kutokomeza ujangili wa Wanyamapori
Akizungumza kwenye mkutano wa tembo unaofanyika leo jijini Dar es Salam kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo wa kimataifa , Mhe. Waziri Nyalandu amesema kwamba mkutano huo utatoa mwelekeo wa jinsi Wizara ya Maliasili na Utalii inakavyoweza kufanya kazi kwa kuuunda kikosi na Wizara hizo ili kuweza kuzuia ujangili na usafirishaji haramu wa Wanyamapori.
Mhe. Nyalandu amesema kwamba kwa kuunda kikosi kazi hicho itasaidia kufanya kazi kwa ushirikiano hivyo kuna uwezekano kuwa tatizo la ujangili likapungua kwa kiasi kikubwa kwa sababu ulinzi kwenye mapori utaimarishwa zaidi ambapo sanjari na hilo Wizara inatarajia kuuajiri tena askari wanyamapori 900.
‘’Maaskari hao wataweza kupunguza tatizo la ujangili na hivyo ulinzi wa wanyamapori utakuwa ni wa uhakika kwa sababu maadili na miiko ya askari wa wanyamapori inatarajiwa kupitia upya kuona jinsi ya kuiboresha ili kuendana na
kizazi hiki cha sasa.’’ Waziri Nyalandu alisema.
Aidha mkutanao huo utajadili jinsi ya kushirikiana na viongozi wa dini kwa kuunda umoja wao ili kuweza kusaidia kukomesha suala la ujangili kwa kutumia viongozi wa dini kuwaasa Waumini wao waache kuwa kushiriki kwenye ujangili wa aina
Pia mkutano huo utaweza kujadili hatua amabayo imefikiwa hadi sasa ya uundaji wa Mamlaka ya Wanyamapori amabyo itaweza kusaidia kuwajibika moja kwa moja kwa kufanya kazi ya kulinda na kuhifadhi wanyamapori.
'
Tunajadili kuona jinsi ambavyo Mamlaka ya Wanyamapori itakavyofanya kazi kwa weledi ya kulinda na kuhifadhi wanyamapori kwa kuajili maaskari wa kutosha na kuwa na utaratibu wa ufanyaji kazi tofauti na sasa.’’ Mhe. Alisisitiza
Mkutano huu ni mwendelezo wa mkutano wa tembo ulifanyika mwezi wa tano mwaka huu ni ikiw lengo ni kuhakikisha tatizo la ujangili linakwisha kwa kushirikana na Wadau wa Maendeleo wakiwemo shirika la Kimataifa la maendeleo ( UNDP).

No comments:

Zilizosomwa zaidi