Monday, September 8, 2014

AJALI YA PIKIPIKI YAUA MMOJA WILAYANI NGARA MKOANI KAGERA

Ajari mbaya ya Pikipiki imetokea eneo la Mugoma jirani na njia ya kuingia kituo cha Polisi  jana Septemba07,2014 ,majira ya saa 11 jioni kwa kuhusisha pikipiki mbili ambapo Madereva  wote  baada ya Ajali kutokea walikuwa katika hali mbaya na mmoja aliyefahamika kwa jina la Jofrey Bangwia kufariki dunia na maziko yake yamefanyika leo Septemba 08,2014 mjini Mugoma huku mwenzake akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Murgwanza.
Aidha Mwanamke aliyekuwa amebebwa na Mumewe aliyefariki dunia alitibiwa majeraha aliyoyapata na kuruhusiwa.
Kwa mujibu wa Mashuhuda wameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi.

No comments:

Zilizosomwa zaidi