Friday, July 11, 2014

MUDA KUOMBA MIKOPO KWA ELIMU YA CHUO KIKUU UMEONGEZWA

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawafahamisha waombaji wa mikopo kwa mara ya kwanza na Umma kwa ujumla kwamba muda wa maombi ya mikopo umeongezwa kwa mwezi mmoja kutoka Julai 1, 2014 hadi Julai 31, 2014.
Bodi ilianza rasmi kupokea maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao kuanzia Aprili 23, 2014 ambapo tarehe ya mwisho wa kupokea maombi hayo ilikuwa Juni 30, 2014.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imetoa muda wa nyongeza kwa waombaji wa mikopo kukamilisha maombi ya mikopo katika kipindi cha siku 30, kupitia mtandao kwa anuani: http://olas.heslb.go.tz

Mwombaji wa mkopo atakayekumbana na matatizo ya kiufundi wakati wa kujaza fomu yake apige simu kwenye dawati la msaada la Bodi kupitia namba 022 550 7910 kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa 2.00 asubuhi hadi saa 2.00 usiku, na Jumamosi kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 10.00 jioni.

Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi hayo kwa njia ya mtandao ni 31 Julai 2014 na hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza baada ya tarehe hiyo kupita.

IMETOLEWA NA: KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

No comments:

Zilizosomwa zaidi