Sunday, July 6, 2014

KUVUJA KWA MKATABA WA KUCHIMBA GESI

Mkataba wa siri wa uchimbaji wa Gesi umevuja,haueleweki namna mapato yatakavyogawanywa kati ya serikali ya kampuni ya Statoil ya Norway iliyopewa tenda ya kuchimba gesi huko Mtwara,kwa majubu wa mkataba huo,mgawanyo huo wa mapato utasababisha Tanzania kupata hasara ya shilingi Trilioni 1.6. kila mwaka,hasara hii ni kwa kitalu namba mbili tu,Tanzania inatajwa kuwa ni kiasi cha gesi asilia trilioni 20,sawa na mapipa bilioni 4 ambacho ni kiwango zaidi ya mafuta yaliyogunduliwa katika nchi za Uganda na Ghana kwa pamoja,
Ndani ya kipindi cha miaka 15 ambacho kampuni ya Statoil kutoka Norway itachimba gesi kwenye kitalu namba mbili,watajikusanyia kiasi cha dola za marekani bilioni 5.6,kumbuka toka Tanzania ipate Uhuru miaka 51 iliyopita,imepatiwa misaada yenye thamani ya dola za marekani bilioni 2.5,huku wakiwa na uhakika wa kukusanya dola bilioni 5.6 ndani ya miaka 15,utaona jinsi hawa wanaojiita wabia wa maendeleo wanavyochota utajili wa Tanzania kwa kisingizio cha kujiita wabia wa maendeleo.
Awali serikali ilisema kuwa kwenye sekta ya gesi,serikali na mwekezaji watagawana asilimia 50 ya mapato,lakini kwa mujibu wa mkataba huo wa gesi kati ya serikali na statoil,mwekezaji atapata asilimia 70 ya mapato huku serikali ikiambulia asilimia 30 tu,kwenye mapato hayo ya gesi.
Mchanganuo huu,ni kwa mujibu wa mkataba wa gesi kati ya serikali na statoil ya Norway uliovuja na kusambazwa mitaandaani.
Na. Bulendu.

No comments:

Zilizosomwa zaidi