Denis Mpagaze-Mwandishi wa makala hii |
Mobutu Sese Seko Kuku
Ngbendu wa Za Banga baada ya kuwa rais wa kwanza Afrika kupata misaada mingi
kutoka USA aliota kiburi na majivuno. Aliitangazia Dunia kwamba yeye ni kuku
anayeatamia nchi ya Congo wakati huo ikiitwa Zaire. Huwezi amini kwa dharau
zake alijifananisha na Mungu. Kabla ya taarifa ya habari, luninga ya Taifa
ilionesha picha yake akishuka kutoka mawinguni na watu wote walikaa kimya
kumlaki mtukufu Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa Za Banga. Ni kufuru. Alijenga
majumba ya kifahari kila kona ya Dunia wakati mamilioni ya wakongo wakiishi
maisha ya Kanyaga Twende. Ni ushenzi. Mwisho wake ulishangaza sana. Alifariki
akiwa uhamishoni Rabat, Morocco kwa ugonjwa wa kansa akiwa na umri wa miaka 66,
na kuzikwa na watu wanne tu. Hili ni funzo kwa viongozi wenye tabia za Mobutu
Seseko. Acheni!
Yuko wapi Saddam Hussein, mbabe aliyoitikisha Dunia mpaka kututia hekaheka ya kuchimba mahandaki kila kona ya nchi yetu. Wengi mnakumbuka. Alitishia kulipua visima vya mafuta ambavyo madhara yake yangekuwa kuiangamiza Dunia. Huu ulikuwa ubabe. Je mnaukumbuka mwisho wake? Pamoja na ubabe wake, alikuja kukamatiwa kwenye shimo mithili ya panya aliyemkimbia paka. Inashangaza na pengine inaweza kuwa funzo kwa viongozi wababe ndani ya nchi yetu kama Saddam. Mbabe siku zote hana rafiki.
Yuko wapi Adolf Hitler aliyemfananisha mtu mweusi na nyani pale alipowashinda wazungu katika mbio za Olympic. Hitler alikataa kumpa mkono jamaa yetu kwa husema haiwezekani binadamu kushindanishwa na nyani. Hii ilikuwa ni kufuru na chukizo kwa Mungu. Nampenda sana hayati Luck Dube, kwa maneno yake matamu, “When I see a black man...I see the image of God, when I see a white man...I see the image of God, I see an Indian...I see the image of God, colours and everybody, we are the images God”, Ni hekima za Lucky Dube .Mwisho wa Hitler nadhani kila mtu anaufahamu. Unashangaza! Hata kaburi lake halijulikani liko wapi. Hili nalo ni funzo kwa viongozi wa namna hii.
Yuko wapi Jonas Savimbi, dikteta wa Angola aliyewakata vidole watoto wetu ili wasije kumpindua madarakani ? Leo vijana wengi huko angola hawana vidole. Ni ubabe huu. Ukiambiwa kifo chake utashangaa. Alifia barabarani na maiti yake kuburuzwa mji mzima kama mzoga wa mbwa kabla ya kuzikwa chini ya mti. Inashangaza. Chukua funzo hili kama ni miongoni mwa viongozi wababe na wenye roho mbaya. Kitendo cha kuuza madawa ya kulevya ni kuwakata vidole watanzania. Acheni!

ITAENDELEA KESHO..
Na Denis Mpagaze
No comments:
Post a Comment