Abiria wote na wahudumu wa ndege ya Air Algerie AH5017 waliangamia jangwani.
Rais wa
Ufaransa Francois Hollande ametangaza kuwa majeshi ya ufaransa
yamefaulu kupata mabaki ya ndege lakini hawakuweza kuokoa nafsi hata
moja.
Aidha
rais Francois Hollande ametangaza kuwa majeshi hao wamepata mtambo wa
kunukuu sauti ''Blackbox'' huko Mali ilikoanguka ndege hiyo iliyokuwa
ikielekea mji mkuu wa Algeria Algiers
Ndege hiyo ilikuwa imetoka mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou ikiwa na Abiria 110 na wahudumu 6 .
Abiria 51 waliokuwa ndani ya ndege hii walikuwa ni raiya wa Ufaransa.
Wengine
walikuwa 27kutoka Burkina Faso, 8 kutoka Lebanon , 6 kutoka Algeria , 2
kutoka Luxembourg, 5 kutoka Canada, Wajerumani 4 .
Jamaa ya wahasiriwa wanakutana huko Ougadougu Burkina Faso
Abiria wengine walikuwa mmoja kutoka mataifa ya Cameroon , Ubeljiji ,Misri Ukraine Uswisi Mnigeria na mmoja kutoka Mali.
Waziri
wa Usalama wa ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve alisema ndege hiyo
iliyokuwa ikielekea Algiers kutoka mji mkuu wa Burkina Faso ,
Ougadougou,ilianguka kutokana na hali mbaya ya anga.
Chanzo:BBC
No comments:
Post a Comment