Muigizaji
mkongwe hapa nchini, Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small
amefariki dunia usiku wa leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili
alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Akithibitisha
taarifa ya kifo cha Mzee Small, mwanae aitwae Mahmoud amesema mzee wake
amefikwa na mauti hayo majira ya saa nne usiku wakati akiwa hospitalini
hapo akiendelea kupatiwa matibabu.
Mipango inafanyika nyumbani kwao Tabata na kadri taarifa zitakavyokuwa zikitufikia tutaendelea kujulishana.
Ni pigo lingine tena kwenye tasnia ya sanaa baada ya kuondokewa na wasanii na kadhaa majuma yaliyopita.
No comments:
Post a Comment