![](http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/06/26/140626093717_luis_suarez_512x288_afp.jpg)
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya
Uruguay Luis Suarez amefungiwa mechi tisa na shirikisho la kandanda
duniani Fifa baada ya kupatikana na hatia ya kumng'ta mlinzi wa timu ya
Italia Giorgio Chiellini kwenye mechi yao ya kombe la dunia nchni
Brazil.
Suarez pia amefungiwa kutojihusisha na shughuli yoyote ya kandanda kwa miezi minne na kutozwa faini ya dola elfu mia moja.
Kutokana na adhabu hiyo Suarez sasa hatashiriki tena kwenye mechi zilizosalia za kombe la dunia ambapo mechi iliyokuwa inafuata raundi ya
pili kati ya Uruguay na Columbia Juni tarehe 28.
Adhabu hiyo pia inamaanisha Suarez hatashiriki
kwenye mechi za Uruguay zijazo za kombe la dunia endapo timu itazidi
kusonga mbele na zile zijazo za kufuzu kwa mashindano ya kombe la dunia.
Kamati hiyo ya nidhamu ya Fifa imesema Suarez
hatakiwi kuingia kwenye uwanja wowote Uruguay inapocheza wakati wa
adhabu hiyo ya kutocheza mechi tisa za kimataifa.
Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya Fifa Claudio
Sulser amesema:"Hatuwezi kuruhusu tabia mbovu kama hii uwanjani hasa
wakati wa kombe la dunia kwani mamillioni ya mashabiki kote duniani
wanafuatilia mashindano haya. Kamati ya Fifa imetilia maanani kila kitu
kwenye kitendo hicho kabla ya uamuzi huo.Tayari tumemjulisha mchezaji
huyo na shirikisho la kandanda la Uruguay.''
Mashabiki wengi duniani wamemshutumu vikali
Suarez kwa kumng'ata mchezaji huyo wa Italia kwani hii ni mara ya tatu
anapatikana na hatia hiyo.
Lakini mashabiki, waandishi wa habari wa Uruguay
na shirikisho la kandanda nchini humo wamemtetea mchezaji wao,wakisema
hizo ni njama za kumuangamiza Suarez ambaye huichezea Liverpool ya
England
No comments:
Post a Comment