Imebainika kuwa, Kaya 75 jijini Mwanza zinatirilisha
vinyesi na majitaka ndani ya Mto Mirongo unaomwaga maji machafu Ziwa Victoria
hali ambayo imedaiwa kuongezaka kwa kasi ya uchafuzi wa mazingira na uharibifu
wa mto huo hivyo kuhatarisha afya ya watumiaji wa maji ikiwemo wanyama, mimea na
viumbe hai waishio majini.
Hali hiyo ilijitokeza na kushuhudiwa na baadhi
ya wadau wa mazingira kutoka Menejimenti ya Ofisi za Maji Bonde la Ziwa
Victoria, Maafisa Afya wa Jiji la Mwanza na Jumuia ya waumiaji wa maji na mazingira
walipokuwa wakifanya zoezi la kufafisha mto Mirongo hii leo ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yanayofanyika jijini humo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo
la daraja la Mabatini linalopitiwa na mto huo baada ya kubaini kuwepo kwa Kaya
hizo, Kaimu Afisa wa Maji kutoka Bonde la Ziwa Victoria Godfrey Kajanja alisema
kwamba, Ofisi yake na Halmashauri ya Jiji zitakutana kuchukua hatua za kisheria
kwa Kaya hizo na watu walio na tabia ya kuchafua maji ya mito.
Kajanja alisema kwamba, hali hiyo ikiendelea
bila kudhibitiwa kutasababisha kuibuka magonjwa ya tumbo endapo Mamlaka ya
Majisafi na Mazingira ya jijini humo haitachukua hatua za kuongeza kiasi
kikubwa cha dawa ya kutibu maji kabla ya kusambazwa kwa watumiaji.
“Lazima sasa tushirikiane kuzitekeleza sheria
zilizopo za Mipango miji kwa upande wa Jiji la Mwanza, pamoja na ofisi yetu ya
Bonde kutumia sheria ya usimamizi wa rasilimali ya maji Na. 11/2009 na sheria
ya usimamizi wa mazingira Na. 24/2004 ambazo zinaoanisha adhabu ya fedha na
kifungo kwa watu watakaokaidi na kukutwa na makosa,” alisema.
Kwa upande wake Mhandisi wa Maji toka ofisi za Bonde
la Ziwa Victoria Mhandisi Jane John alieleza kwamba, hatua hivyo inatakiwa
kukomeshwa mara moja na jamii iliyo kandokando ya maeneo unapipita mto Miringo
na maeneo ya vyanzo vya maji ili kusaidia kulinda na tabia ya uchafuzi wa
mazingira ikiwemo udhibiti jambo ambalo litaepusha uharibifu na uchafuzi.
“Tumeshuhudia mabomba ya vinyesi na maji machafu
yakimwaga mtoni wakati tukifanya usafi wa pamoja kwenye mto Mirongo na wadau
mbalimbali walioko kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira kitaifa hili ni
jambo ambalo linahitaji hatua za haraka kulikomesha na kuwachukulia hatua
wanaofanya uchafuzi huu,”alisisitiza.
Naye Mwenyekiti wa NGO ya Jumuiya ya watumiaji maji
na mazingira Adam Shija ya Kata ya Mbugani Wilayani Nyamagana mkoani hapa
alisema kwamba, tumekuwa na changamoto kubwa wakati wa usafishaji wa mto huo na
wamebaini kuwepo kwa baadhi ya Kaya 75 ambazo zimekuwa zikitirilisha uchafu wa
vinyesi na majimachafu ndani ya mabomba yaliyoelekezwa mtoni humo.
Shija alifafanua walipotembelea kandokando yam to
huo kwenye maeneo ya unapoanzia na kupitia kasha kumwaga maji ziwani Victoria
katika Kata za Nyakato walibaini kaya 16, Mahina kaya 8, Mbugani kaya 24,
Mirongo kaya 17, Nyamagana kaya 6 na Pamba kaya 4 na tayari orodha hiyo
imetokana na ukaguzi wa Jumuiya hiyo hivi karibuni.
Wito wangu kwa Serikali na Idara zenye jukumla la
kusimamia rasilimali ya maji na mito, mabwawa na ziwa Victoria kutekeleza
sheria kwa vitendo ili kukomesha tabia hiyo ya uchafuzi wa maji na uharibifu wa
mazingira unaofanywa kwa makusudi na baadhi ya wananchi bila kujali kama
husababisha madhala kwa watumiaji wa maji na kuhatarisha uhai wa viumbe hai majini.
No comments:
Post a Comment