Polisi
nchini Tanzania wamewakamata waganga wawili wa kienyeji baada ya
mwanamke mmoja mwenye ulemavu wa ngozi au Abino kuuwawa kwa kuchinjwa.
Moja ya
miguu yake pamoja na vidole vilinyofolewa baada ya shambulizi hilo la
hapo jana Jumanne katika mkoa wa Simiyu Kaskazini Mashariki mwa
Tanzania. Kumekuwa na visa vingi vya mauaji ya albino katika eneo hilo
hapo awali.
Shirika
la kutetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi Albino la 'Under the
Same Su'n limeiomba serikali ya nchi hiyo kufuta vibali na shughuli zote
za waganga wa jadi kwa madai kuwa wao ndiyo chanzo cha kuuawa kwao.
Kuuawa
kwa mwanamke Munghu Lugata mlemavu wa ngozi toka kijiji cha Gasuma
mkoani Simiyu Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo kumeacha hisia na
uchungu kwa walemavu wengine waliopata mikasa hiyo.
Akizungumza
na mwandishi wa BBC Leonrad Mubali kwa uchungu na kilio, Mariamu
Staford mlemavu wa ngozi Albino amesema kwamba tukio la kuuawa kwa
Munghu Lugata mwanamke mwenye umri wa miaka 40 juzi linamkumbusha mkasa
wake uliomkuta wa kukatwa mikono yake yote, zaidi ya miaka mitano
iliyopita na sasa anatumia mikono ya bandia ya vyuma huku akisema
malengo yake mengi yamekwama.
Albino
wamekuwa wakihangaishwa sana nchini Tanzania ambako baadhi ya watu
wanaamini kuwa dawa za miujiza zinazotengezwa kutokana na viungo vya
miili yao zinaleta bahati nzuri.
Mashambulizi
yamepungua katika siku za hivi karibuni lakini mauaji ya hivi punde
yamepelekea shirika moja la kutetea haki za Albino kutoa wito kwa
serikali kupiga marufuku waganga wote wa kienyeji.
Matukio
mengi ya maujia ya walemavu nchini Tanzania yamekuwa yakihusishwa na
imani za kishirikina huku waganga wa jadi wakihusishwa.
Mkoa wa Simiyu ni moja katika maeneo kaskazini magharibi mwa Tanzania yenye matukio mengi ya mauaji hayo.
Hivi
karibuni nchini Tanzania umezinduliwa mnara maalumu unaoitwa NITHAMINI,
mnara pekee duniani unaowakilisha kupinga mauaji ya albino huku Tanzania
ikiwa ni moja ya nchi yenye matukio mengi ya ukatili dhidi ya walemavu
hao
Chanzo:BBC
No comments:
Post a Comment