WATU
10 wamekufa na wengine 10 kujeruhiwa baada ya basi dogo la abiria
walilokuwa wakisafiria kugonga lori lililokuwa na kokoto lililoegeshwa
kando ya barabara kisha kupinduka katika eneo la Nyamhongholo, jijini
Mwanza.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika hospitali ya Rufaa ya Bugando, Daktari wa
Idara ya Dharura, Dk Regina Mutayangulwa, alisema miili ya abiria hao
na majeruhi walipokewa hospitalini hapo juzi usiku.
Majeruhi
waliolazwa katika wodi za upasuaji ni pamoja na wanawake watatu
waliolazwa katika wodi namba 9C na wanaume saba waliolazwa katika wodi
namba 6Cna 8E na hali zao zinaendelea vizuri.
Waliojeruhiwa ni pamoja na
Verynice Protas (22), Rosemary Petro (26), Prisca Peter (25), Hamad
Haruna (22) ambaye amevunjika mkono wa kushoto na paji la uso kuharibika
na Benson Joseph (27).
Wengine ni Nyanda Sahani, Magesa Musa (30), Rushinge Nyerere, Japhet Mlangwa (23) na Shija Nyanda Ngwenda.
Akizungumzia ajali hiyo,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentine Mlowola, alisema ilitokea
Mei 13 saa moja usiku katika Barabara Kuu ya Mwanza- Musoma.
Alisema ajali hiyo ilihusisha
gari lenye usajili namba T 769 CQE aina ya Toyota Coaster, lililokuwa
likiendeshwa na Yohana Mayandakia likitokea Mwanza kwenda Bunda, ambapo
liligonga Lori aina ya Iveco, lenye namba T832 AEF na tela namba T 187
AEF.
Alisema lori hilo lilikuwa limeegeshwa pembeni mwa barabara na dereva aliyeitwa Emmanuel Zakaria (33) ambalo lilikuwa bovu.
Kamanda Mlowola alisema chanzo
cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva kutokuwa mwangalifu na ishara
iliyokuwa imewekwa mbele ya gari lililokuwa bovu. Dereva wa lori
anashikiliwa na Polisi kwa uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment