![]() |
Baadhi ya majeruhi katika mlipuko wa bomu uliotokea Arusha wakiwa hospitali. |
WATU
waliohusika na kutega bomu linalohisiwa kuwa ni la kienyeji katika baa
ya Arusha Night Park huenda wakanaswa kirahisi baada ya polisi kuchukua
mitambo ya usalama (CCTV) iliyofungwa kwa ajili ya kufanya uchunguzi
Katika
tukio hilo lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita, jumla ya watu 17
walijeruhiwa, baadhi yao vibaya sana wakati wakinywa na kufuatilia
katika televisheni michuano ya soka inayochezwa katika nchi mbalimbali
barani Ulaya.
Kamanda
wa polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas aliyefika eneo la tukio haraka
akiwa na kikosi cha ukaguzi wa mabomu, mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa
Mulongo na wa wilaya ya Arusha, John Mongella walishuhudia majeruhi
wakiondolewa na kupelekwa katika hospitali mbalimbali kwa ajili ya
kupatiwa matibabu.
Mmiliki
wa baa hiyo, Joseph Karugendo alisema anaamini waliohusika na tukio
hilo lililojeruhi wafanyakazi na wateja wao watapatikana kwani walifunga
mitambo ya kufuatilia matukio ya CCTV.
“Baada ya tukio lile polisi walifika, wakazingira eneo lile hivyo leo
asubuhi (juzi) polisi wameondoka na ‘monitor’ ya CCTV pamoja na mfanyakazi wetu mmoja kwa lengo la kwenda kufanyia uchunguzi wa picha hizo,” alisema mkurugenzi huyo.
asubuhi (juzi) polisi wameondoka na ‘monitor’ ya CCTV pamoja na mfanyakazi wetu mmoja kwa lengo la kwenda kufanyia uchunguzi wa picha hizo,” alisema mkurugenzi huyo.
Mmoja
wa wahudumu waliokuwepo wakati tukio hilo likitokea, Aneth Mushi,
alisema alikuwa amebeba chakula cha wateja ndipo aliposikia kishindo
kikubwa na kelele za watu zilizomfanya aangushe sahani za chakula na
kukimbia.
“Kwa
kweli nasikitika sana watu wameumia na mimi ni Mungu tu kaniokoa
vinginevyo ningeweza kuwa mmoja wa majeruhi,” alisema Aneth.
Hili ni tukio la tatu la bomu kutokea kwenye Jiji la Arusha kwa kipindi cha
mwaka mmoja ambapo jumla ya watu saba wamepoteza maisha huku wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa.
mwaka mmoja ambapo jumla ya watu saba wamepoteza maisha huku wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa.
Katika
tukio la Mei 5, mwaka jana bomu lilirushwa kwenye Kanisa laKatoliki la
Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Olasiti ambapo jumlaya watu
watatu walifariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Tukio la pili ni lile la Juni 15, mwaka jana ambapo bomu lilirushwa kwenye
mkutano wa kufunga kampeni wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) kwenye Viwanja vya Soweto ambapo jumla ya watu wanne walifariki dunia akiwemo mwanamke mmoja na watoto watatu.
Hata hivyo tayari mtu mmoja amefikishwa mahakamani kuhusiana na tukio la bomu kanisani.

No comments:
Post a Comment